KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 20, 2010

TULICHEZA OVYO !!!!!


Meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson amesema hawakucheza vizuri katika mchezo wa jana wa ligi ya Ulaya walipokutana na klabu ya Trabzonsporya toka nchini Uturuki.

Roy Hodgson amesema kufuatia hatua hiyo kikosi chake kikipoteza nafasi nyingi za wazi na kumaliza dakika 90 kwa ushindi wa bao moja kwa sifuri ambao bado ni hatari kwao wakaposafiri hadi nchini Uturuki juma lijalo.

Amesema kikosi chake endapo kingecheza vizuri kilikua na sababu zote za kupata bao la pili na la tatu lakini hatua hiyo ilishindikana kufuatia kukosekana kwa umakini kwa baadhi ya wachezaji wake.

Mbali na hatua hiyo pia meneja huyo wa kimataifa toka nchini Uingereza ameongeza kwamba, kitendo cha kukosa penati kwa kiungo wake Joe Cole pamoja na kile cha bao la Christian Poulsen kukataliwa na muamuzi huenda kilichangia kuwashusha morari wachezaji wake.

Bao pekee na la ushindi la Liverpool katika mchezo huo limefungwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uholanzi Ryan Babel katika dakika 45.

No comments:

Post a Comment