KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 12, 2010

TULISTAHILI KUSHINDA.


Kikosi cha timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana usiku wa kuamkia hii leo kimemfurahisha kocha wa timu hiyo Pitso Mosimane, alierejea kuifundisha timu hiyo mara baada ya mkataba wa aliekua kocha Carlos Alberto Perreira kumalizika mwishoni mwa fainali za kombe la dunia.

Bafana Bafana wamekamilisha malengo ya Pitso Mosimane mbele ya mashabiki wa Afrika kusini waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Soccer City kwa kuifunga timu ya taifa ya Ghana bao moja kwa sifuri.

Bao hilo pekee na la ushindi la Bafana Bafana, limepachikwa wavuni na mshambuliaji wa klabu ya Mamelodi Sundowns Katlego Mphela katika dakika ya 42.

Mara baada ya mchezo huo Katlego Mphela alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari na kusema walikua na kila sababu za kushinda mchezo wa jana na kwa bahati nzuri wametimiza suala hilo ambalo lilikua likisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Afrika kusini.

Amesema mbali na kupata bao la ushindi katika kipindi cha kwanza bado walikuwa na nafasi ya kupata bao lingine katika kipindi cha pili lakini kasi ya wachezaji waliochukua nafasi za wengine hawakuwa fit.

No comments:

Post a Comment