KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 17, 2010

UEFA CHAMPIONS LEAGUE.


Michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya inatarajiwa kuendelea hii leo kwa michezo ya kwanza ya hatua ya mtoano kuchezwa kwenye viwanja tofauti barani humo.

Macho na masikio ya mashabiki wa soka nchini uingereza yanatarajiwa kuelekezwa huko nchini Uswiz kwenye uwanja wa Wankdorf, ambapo Tottenham Hotspours watakaribishwa na wenyeji wao BSC Young Boys.

Harry Rednapp meneja wa Tottenham Hotspours ameshajinadi kupitai vyombo vya habari kwa kusema kwamba endapo atapoteza mchezo wa hii leo kwake halitokua dhoruba kufuatia kuwa na nafasi nyingine katika mchezo wa pili utakaochezwa nchini Uingereza juma lijalo.

Meneja huyo wa kimataifa toka nchini Uingereza pia amesema anatarajia kuwakosa baadhi ya wachezaji wake katika mchezo huo kufuatia majeraha yanayowakabili.

Jermaine Jenas Ledley King David Bentley , Jamie O'Hara pamoja na Jonathan Woodgate.

Spurs squad: Gomes, Cudicini, Hutton, Bale, Kaboul, Naughton, Bassong, Dawson, Corluka, Assou-Ekotto, Walker, Huddlestone, Rose, Lennon, Palacios, Modric, Kranjcar, Pavlyuchenko, Keane, Crouch, Dos Santos, Defoe.

Michezo mingine ya michuno hiyo;

Petrovski Stadium
Zenit St Petersburg (urusi) v AJ Auxerre (Ufaransa)

Valeri Lobanovski Stadium
Dynamo Kiev (Ukraine) v Ajax Amsterdam ( Uholanzi)

Lerkendal
Rosenborg (Norway) v FC Copenhagen (Denmark)

AXA Arena
Sparta Prague ( J.Czech) v MSK Zilina (Slovakia)

No comments:

Post a Comment