KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 26, 2010

VIJANA WALISTAHILI.


Baada ya kufanya kweli kwenye mchezo wa jana wa hatua ya mtoano dhidi ya klabu ya Young Boys toka nchini Uswz na kutinga kwenye hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, Meneja wa klabu ya Tottenham Harry Redknapp amesema kikosi chake kilistahili kupata mafanikio hayo.

Harry Redknapp amesema umakini wa wachezaji wake ulikua kigezo tosha cha kutoa sifa hizo kwa wachezaji wake ambao walionyesha njaa ya kusaka mabao katika mchezo huo mbao walitakiwa kushinda ili wasonge mbele.

Amesema walikua na wakati mgumu kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa juma lililopita huko nchini Uswiz na mwisho wa mchezo huo walijikuta wakipoteza kwa kubamizwa mabao matatu kwa mawili dhidi ya wapinzani wao Young Boys.

Nao mashabiki wa klabu hiyo ya jijni London kwa nyakati tofauti walionekana wakishangilia ushindi wa mabao manne walioupata jana ambao unawapelekea kwenye hatua ya makundi la ligi ya mabingwa.

Mashabiki hao wamesikika wakisema umewadia wakati wa kushindana na klabu kubwa kama Real Madrid, AC Milan, Fc Barcelona na klabu nyingine baada ya kushiriki michuano ya ligi ya Ulaya msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment