KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 12, 2010

WANASTAHILI SIFA.


Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amekisifia kikosi chake mara baada ya kufanya vyema kwenye mchezo wa kujipima nguvu uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya timu ya taifa ya Hungary.

Fabio Capello amesema kikosi chake kilichokua kimesheheni damu changa kwa hakika kimeonyesha mchezo wa kujiaminia ambao anaamini ulikuwa chanzo cha kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya timu ya taifa ya Hungury.

Katika mchezo timu ya taifa ya Uingereza ilipata mabao yake kupitia kwa Steven Gerrard katika dakika 70 na 73 huku Philly Jagielka akiizawadia bao Hungary katika dakika ya 62.

Meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italia amesema bado ataendelea kuwa na kikosi hicho cha vijana kwenye michezo ya kuwani kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2012.


No comments:

Post a Comment