KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 24, 2010

YOANN GOURCUFF AJIUNGA NA OLYMPIQUE LYONNAIS


Mabingwa wa zamani nchini ufaransa Olympique Lyonnais wamewashiwa taa ya kijani na uongozi wa klabu ya Girondins de Bordeaux katika harakati zao za kumsajili kiungo Yoann Gourcuff kwa ada ya uhamisho wa Euro million 22.

Taa ya kijani kwa Olympique Lyonnais imewashwa kufuatia kukamilika kwa mazungumzo ya uongozi wa vilabu hivyo viwili na kuanzi hii leo dili la mchezaji huyo huenda likakamilishwa.

Kabla ya kukamilishwa kwa mazungumzo hayo Gourcuff alikuwa anasemekana huenda angesalia katika klabu yake ya Girondins de Bordeaux kwa msimu mwingine baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kuisaidia klabu hiyo msimu uliopita.

Hata hivyo taarifa nilizozipata hivi sasa zimenifahamisha kwamba Yoann Gourcuff amekamilisha taratibu za kujiunga na Olympique Lyonnais.

No comments:

Post a Comment