KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 27, 2011

AC MILAN WAJIENGUA KWA FABREGAS, ARSENAL WAMTAKA FALCAO.


Makamu wa raisi wa mabingwa wa soka nchini Italia AC Milan, Adriano Galliani ametangaza kuiondoa klabu hiyo katika mbio za kumuwania nahodha na kiungo wa klabu ay Arsenal, Francis Cesc Fabregas ambae yu mbioni kuondoka huko Emirates.

Adriano Gallian ametangaza mpango huo huku akikiri kwamba gharama ya kiungo huyo ni kubwa na katu klabu yao haiwezi kuimudu hivyo wanaona ni bora waendelee kusaka wachezaji wengine ambao wana gharama wanayoweza kuimudu.

Amesema ukweli ni kwamba wanatamani kiungo huyo ajiunge na klabu hiyo ya San Siro lakini hawana budi kukubaliana na hali halisi iliopo sasa hasa ikizingitiwa asilimia ya wachezaji wengi gharama yao imekuwa kubwa katika siku za hivi karibuni.

Adriano Galliani ambainisha kwamba kufuatai kujiondoa katika mbio za kumsajili Fabregas, sasa macho yao wanayaelekeza kwa kiungo wa klabu ya Napoli Marek Hamsik ambae anafananishwa na Fabregas kiuchezaji.


Wakati huo huo wakala wa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Colombia pamoja na klabu ya FC Porto Radamel Falcao, amesema uongozi wa klabu ya Arsenal pamoja na Tottenham umetuma ofa ya kutaka kumsajili mchezaji huyo.

Claudio Mossio wakala wa mshambuliajhi huyo alietamba katika msimu wa mwaka 2010-11 katika ligi ya nchini Ureno pamoja na kwenye michuano ya ligi ya barani Ulaya amesema bado haijafahamika ni wapi Radamel Falcao atakapoelekea lakini tayari ada yake ya uhamisho imetajwa kuwa ni paund million 26.

Radamel Falcao msimu wa mwaka 2010-11 amefanikiwa kupachika mabao 41 katika michezo 39 aliyocheza na katika mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya barani Ulaya alifunga bao la ushindi dhidi ya Fc Braga.

No comments:

Post a Comment