KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, May 28, 2011

AKIFANIKIWA LEO NA KAZI BASI.


Gwiji wa soka nchini Uholanzi Johan Cruyff amesema meneja wa klabu bingwa nchini Hispania Josep Pep Guardiola Isala huenda akaachana na klabu hiyo mara baada y mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya utakayochezwa usiku huu dhidi ya Manchester United, huko jijini London nchini Uingereza.

Johan Cruyff amesema Guardiola mwenye umri wa miaka 40, anahisiwa huenda akaacha shughuli ya kukinoa kikosi cha klabu hiyo endapo atafanya jitihada ya kuweka historia ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa kuifunga Man utd mara ya pili mara baada ya kufanya hivyo mwaka 2009 kule nchini Italia katika mji wa Roma.

Mzee huyo wa kidachi mwenye umri wa miaka 64 ambae pia ni raisi wa kudumu wa klabu ya Barcelona, ameongeza kwamba Josep Pep Guardiola amekua akifanya kazi kwa jitihada ili aweze kuyafikia malengo aliyojiwekea na kubwa ni kuhakikisha anatwaa ubingwa wa barani Ulaya usiku huu.


Hata hivyo amedai kwamba endapo meneja huyo ataondoka huenda kukatanda wingu zito huko Camp Nou la kuamua nani atachukua nafasi yake, licha ya taarifa kudai kwamba huenda mshambuliaji wa zamani wa kiholanzi Marco van Basten akapewa jukumu la umeneja.

Ikumbukwe kwamba Josep Pep Guardiola Isala, wakati akiitumikia klabu ya Barcelona toka mwaka 1990–2001 aliwahi kufundishwa na Johan Cruyff toka mwaka 1990–1996 na pamekua na mawasiliano mazuri kati ya wawili hao hivyo inahisiwa siri hiyo ya kuachia ngazi mara baada ya mchezo wa hii leo alielezwa mzee huyo.

No comments:

Post a Comment