KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 17, 2011

Alexis Alejandro Sánchez ASAKA KWA UDI NA UVUMBA !!


Uongozi wa klabu ya Udinese umesisitiza jambo la kutokua tayari kuwauza wachezaji wake muhimu endapo klabu hiyo itafanikiwa kupata nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.

Msisitizo wa uongozi wa klabu hiyo ya huko Stadio Friul umekuja kufuatia taarifa zilizoshamiri katika vyombo vya habari vya nchini Italia pamoja na nchini Uingereza ambazo zinadai kwamba klabu za FC Barcelona, Chelsea, Galatasaray, Internazionale, Liverpool, Manchester United, pamoja na Manchester City zipo mbioni kutuma ofa ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Chile pamoja na klabu hiyo Alexis Alejandro Sánchez.

Katika msimamo wa ligi ya nchini Italia *SIRIE A* unaonyesha kwamba Udinese wapo katika nafasi ya nne wakiwa mbele kwa idadi ya point mbili dhidi ya Lazio huku wakiwa wamesalia na mchezo mmoja wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya AC Milan.

Endapo Udinese watafanikiwa kushinda mchezo huo watafikisha point 68 na kujihakikishia nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment