KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 23, 2011

ANCELOTTI HAKUFAHAMU LOLOTE ZAIDI YA KUTARAJIA MKUTANO!!


Imefahamika kwamba aliekua meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Michelangelo Ancelotti alikua hafahamu lolote juu ya hatua ya kutimuliwa kwake zaidi ya kutambua mpango wa kuwepo kwa mkutano kati yake na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.

Carlo Michelangelo Ancelotti alionyesha hatua hiyo mara baada ya mchezo wa mwisho wa ligi msimu huu, kati ya kikosi chake dhidi ya Everton kumalizika huko Goodson Park ambapo alisema hana budi kusubiri kikao ambacho kitaamua mustakabali wa maisha yake ya baadae huko Stamford Bridge.

Ancelotti pia alikua hana hakika kama angeendelea kusalia klabuni hapo kufuatia kukiri yeye mwenyewe kwamba msimu huu matokeo hayakua mazuri kwake mbali na msimu uliopita hivyo alitarajia lolote katika mkutano huo na bosi Abramovich.

Maamuzi ya kutimuliwa kazi kwa meneja huyo wa kimataidfa toka nchini Italia yalichukuliwa akiwa safarini akitokea mjini Liverpool sambamba na kikosi cha klabu ya Chelsea ambacho kilikua kikirejea jijini London.

Taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye mtandao wa klabu ay Chelsea imeeleza kwamba Ancelotti ametimuliwa kazi kufuatia matokeo mabovu yaliyokiandama kikosi chake mwishoni mwa mwaka jana hatua ambayo ilipelekea klabu hiyo kupoteza muelekeo wa kutetea ubingwa.

Pia taarifa hiyo imedai kwamba mbali na kupoteza muelekea wa kutetea ubingwa wa nchini Uingereza, meneja huyo alishindwa kukiwezesha kikosi chake kufanya vyema katika michuano mingine waliyoshiriki ikiwa ni pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.


Hata hivyo Ancelotti ataendelea kukumbukwa klabuni hapo baada ya kuiwezesha Chelsea kutwaa ubingwa wa kombe la ligi msimu uliopita sambamba na kombe la chama cha soka nchini Uingereza FA hatua ambayo ilimfanya kuonyesha furaha mwishoni mwa msimu uliopita tena kwa kuimba nyimbo mbali mbali walipokua wakipita mitaani kwa ajili ya kushangilia ubingwa walioupata.

Solomon Kalou mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast ameelezea masikitiko yake baada ya Carlo Ancelotti kupokea taarifa za kufungashiwa viwago huko jijini London.

Hata hivyo amedai kwamba walikua hawafahamu lolote juu ya kutimuliwa kwake lakini ametoa wito kwa wachezaji wenzake kuutumia vyema muda wa mapumziko kabla hawajakutana tena mwezi July tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

1 comment:

  1. Mzee wa libeneke vipi?
    Upo kweli?au upo mapumzikoni kidogo?
    Naona blog yetu imesinzia kidogo.
    Asante ,ni mdau wa blog hii from The Hague.

    ReplyDelete