KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, May 21, 2011

Andrea Pirlo KUONDOKA, Massimo Ambrosini AKUBALIA KUBAKI.


Baada ya kugoma kusaini mkataba mpya, kiungo wa kimataifa toka nchini humo pamoja na klabu bingwa ya “Sirie A” msimu huu AC Milan Andrea Pirlo imeeleza kwamba yu mbioni kujiunga na klabu ya Juventus yenye maskani yake makuu huko Stadio Olimpico di Torino.

Taarifa za harakati za kiungo huyo kuelekea Juventus kwa ajili ya msimu mpya wa ligi, zimeelezawa wazi na rafiki yake wa karibun aitwae Tullio Tinti baada ya kukaririwa na gazeti la kila siku la michezo la nchini Italia liitwalo "Gazzetta dello Sport " ambapo amesema mipango ya Andrea Pirlo ni kutaka kuichezea klabu hiyo kongwe.

Tullio Tinti amesema siku kadhaa zilizopita Andrea Pirlo alimueleza wazi kwamba angetamani sana kujiunga na meneja wake wa zamani Carlo Ancelotti huko nchini Uingereza katika klabu ya Chelsea lakini hali ya sintofahamu iliyotanda kwa meneja huyo imemkwamisha kutimiza ndoto yake.


Wakati huo huo kiungo wa kimataifa toka nchini Italia pamoja na klabu ya AC Milan Massimo Ambrosini amekubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambao utafikia kikomo mwezi June mwaka 2012.


Hata hivyo uongozi wa klabu ya AC Milan bado umeripotiwa kuendelea na mazungumzo ya kumbembeleza kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi Clarence Seedorf ili aweze kukubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja kufuatia mkataba wake wa sasa kuwa mbioni kufikia kikomo.

No comments:

Post a Comment