KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 31, 2011

Andriy Shevchenko KUSTAHAFU SOKA MWAKA 2012.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ukraine pamoja na klabu ya Dynamo Kiev Andriy Shevchenko amesema atastahafu soka mara baada ya fainali za mataifa ya bara la Ulaya za mwaka 2012 ambazo zitafanyika nchini kwao kwa ushirikiano na nchi ya Poland.

Shevchenko, ameweka wazi mustakabali huo wa maisha yake katika soka alipohojiwa na gazeti la kimichezo la kila siku la nchini kwao Ukraine liitwalo La Repubblica, ambapo amesema bado ana hamu ya kuendelea kuitumikia timu ya taifa lake pamoja na klabu ya Dynamo Kiev ambayo ilimkuza toka akiwa na umri wa miaka 10.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, amesema maamuzi yake ya kufikiria kuacha soka mara baadaya fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka ujao, anatarajia kuyafanya baada ya kusaka ushauri kutoka katika familia yake ambayo pia imekua ikimpa ushirikiano wa kutosha.

Mpaka sasa Andriy Shevchenko ameishaitumikia timu ya taifa ya Ukraine kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita na amecheza michezo 100 huku akifanikiwa kupachika mabao 45.

No comments:

Post a Comment