KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 24, 2011

ARSENE AAHIDI KUFANYA USAJILI WA WACHEZAJI.


Hatimae meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amekubalia kutumia fedha kwa ajili ya kufanya usajili wa wachezaji ambao anaamini wataongeza chachu ya kupatikana kwa mafanikio ndani ya kikosi chake ambacho kimeshasota kwa muda wa msimu sita bila ya kuwa na mafanikio yoyote.

Wenger amekiri kufanya hivyo, huku akiendelea kushikilia msimamo wake wa kutotumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kumsajili mchezo mmoja ama wawili ambapo amesema utaratibu huo ni wa kijinga na wa kipuuzi.

Amesema suala la kutumia fedha nyingi kumsajili mchezo mmoja ama wawili halimaanishi upatikanaji wa mafanikio, zaidi ya kujipanga na kutambua kufanya mikakati ambayo itamsaidia kwa msimu mzima wa ligi.

Katika hatua nyingine uongozi wa klabu ya Arsenal umetangaza kufanya ziara nchini Malaysia ikiwani sehemu ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi wa mwaka 2011-12.

Mtendaji mkuu wa klabu ya Arsenal Ivan Gazidis amesema ziara hiyo ya nchini Malaysia itafanyika mwezi July na kikosi cha Arsene Wenger kikiwa nchini humo kitacheza mchezo mmoja ambao utakuwa dhidi ya kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kitakua kikijiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya Taiwan July 23.

Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki utafanyika katika uwanja wa Bukit Jalil ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 80,000 walioketi.

Kwa mara ya mwisho Arsenal walifanya ziara nchini Malaysia mwaka 1999, ambapo wakati huo walikwenda mjini Kuala Lumpur.

No comments:

Post a Comment