KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 23, 2011

BAHATI YA MTENDE IMETUANGUKIA.


Meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini amekiri kwamba hatua ya kikosi chake kumaliza kwenye nafasi tatu za juu katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu huu ameichukulia kama bahati ya mtende iliyowaangukia.

Mancini aliekabidhiwa kikosi cha klabu hiyo mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kutimuliwa kazi Mark Hughes huko City Of Manchester amesema ni vigumu kuamini lakini hana budi kukubaliana na hali halisi kwani majuma mawili yaliyopita alikua hadhani kama wangemaliza na kufikia walipo hivi sasa.

Amesema juhudi za kikosi chake pamoja na kuhizana kila wakati imekua ni hatua kubwa kwao kufikia malengo waliyojiwekea hivyo kwa sasa wanajipanga kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya tena wakianzia katika hatua ya makundi.

Man city wamefanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Bolton Wanderers mabao mawili kwa sifuri huko Reebok Stadium huku Arsenal wakilazimisha sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Fulham huko Craven Cottage.

Katika hatua nyingine Roberto Mancini amesema bado anaamini mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez ataendelea kubaki huko City Of Manchester licha ya kuwepo kwa taarifa za kutatanisha.

Mancini amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 bado ana mkataba wa muda mrefu hivyo imani yake yamtuma ataendelea kubaki.

Carlos Tevez mwishoni mwa juma lililopita alieleza wazi kwamba atakuwa mwenye furaha zaidi endapo ataondoka Manchester City na kusaka sehemu nyingine ambayo itamuwezesha kupata changmoto mpya katika soka lake baada ya kuipa mafanikio klabu hiyo ya City Of Manchester.

No comments:

Post a Comment