KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 27, 2011

Birmingham City WAACHA MILANGO WAZI KWA WANAOTAKA KUONDOKA.


Uongozi wa klabu ya Birmingham City umethibitisha taarifa za kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo baada ya kushuka daraja kutoka ligi kuu ya soka nchini Uingereza hadi katika ligi daraja la kwanza mwishoni mwa juma lililopita.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo ya mjini Birmingham imeeleza kuwa msimu ujao wachezaji kama Kevin Phillips, Sebastian Larsson, Maik Taylor, Martin Jiranek, Stuart Parnaby pamoja na Lee Bowyer hawatokuwepo klabuni hapo.

Sababu kubwa za wachezaji hao kuonyeshwa mlango wa kutokea ni kufuatia mikataba yao kufikia kikomo hatua ambayo imepelekea kushindwa kufungua mazungumzo mapya ya kuongeza mikataba mingine kutokana na wachezaji hao kuhitaji changamoto mpya.

Wakati wachezaji hao wakionyeshw amlango wa kutokea uongozi wa Birmingham City umekubali kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja nahodha Stephen Carr huku mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Scotland ambae alikosa sehemu msimu wa mwaka 2010-11 kufuatia maumivu ya goti James McFadden akiwa katika mazungumzo ya kutaka kuongeza mkataba mpya.

No comments:

Post a Comment