KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 30, 2011

Bixente Lizarazu AAHIDI KUTEMBEA BARABARANI AKIWA MTUPU.


Beki wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa pamoja na klabu ya Bayern Munich Bixente Lizarazu ametangaza kushangilia ubingwa wa klabu ya mji anaoishi ya Evian ambayo imefanikiwa kupanda daraja msimu huu ambapo itacheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Bixente Lizarazu ametangaza kushangilia ubingwa wa klabu hiyo kwa kutembea katika mitaa ya mji wa Evian akiwa mtupu hatua ambayo amesema ataichukulia kama kuonyesha furaha yake ailiyo nayo moyoni.

Amesema hakuna kinacho shindikana katika suala hilo na hakuna atakaeweza kumzuia hivyo amewataka mashabiki wa soka nchini humo pamoja na wale wa klabu ya Evian kusubiri na kuona namna atakavyoikamilisha furaha yake.

Lizarazu anakumbukwa kwa mazuri aliyoyafanya akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa ambacho kilitwaa ubingwa wa dunia katika fainali za mwaka 1998 pamoja na ubingwa wa barani Ulaya mwaka 2000 kabla ya kufanya maamuzi ya kustahafu soka mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment