KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 24, 2011

Bobby Zamora AITWA KIKOSINI.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza pamoja na klabu ya Fulham Bobby Zamora amerejeshwa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kitaingia kambini tayari kwa kuanza maandalizi ya mchezo wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya dhidi ya Uswiz.

Zamora anarejeshwa kikosini baada ya kuitwa kwa mara ya mwisho mwezi August mwaka jana katika mchezo wa kimataifa dhidi ya Hungary, na hii ilitokana na hatua ya kuvunjika mguu akiwa na klabu yake ya Fulham hali ambayo ilimuweka nje kwa kipindi kirefu kilichopita.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amefanya maamuzi ya kumuita mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, kwa lango la kuziba nafasi ya mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Andy Carroll ambae ni majeruhi pamoja na Wayne Rooney ambae anatumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi mbili za njano hivyo hatoruhusiwa kucheza mchezo dhidi ya Uswiz.

Kikosi kamili cha timu ya taifa ya Uingereza kilichoitwa na Fabio Capello kwa upande wa

Makipa: Joe Hart (Manchester City), Scott Carson (West Bromwich Albion), David Stockdale (Fulham)

Mabeki: Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Bolton Wanderers), Ashley Cole (Chelsea), Rio Ferdinand (Manchester United), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Joleon Lescott (Manchester City), John Terry (Chelsea), Kyle Walker (Tottenham Hotspur)

Vungo: Gareth Barry (Manchester City), Michael Carrick (Manchester United), Stewart Downing (Aston Villa), Adam Johnson (Manchester City), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Manchester City), Scott Parker (West Ham United), Theo Walcott (Arsenal), Jack Wilshere (Arsenal), Ashley Young (Aston Villa)

Washambuliaji: Darren Bent (Aston Villa), Peter Crouch (Tottenham Hotspur), Jermain Defoe (Tottenham Hotspur), Bobby Zamora (Fulham)

No comments:

Post a Comment