KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 17, 2011

Brendan Rodgers ATANGAZA VITA WEMBELY STADIUM.Siku moja baada ya ushindi wa mabao matatu kwa moja uliopatikana mbele ya Nottingham Forest meneja wa klabu ya Swansea Brendan Rodgers ametamba kufanya vyema katika mchezo hatua ya fainali ya ligi daraja la kwanza itakayofanyika May 30 katika uwanja wa Wembely jijini London.

Brendan Rodgers aliekiongoza kikosi cha Swansea kwa muda wa Mwaka mmoja na nusu ametamba kufanya vyema katika mchezo huo huku akiamini hakuna mabadiliko yoyote ya sehemu ya kuchezea watakayoyakuta katika uwanja wa Wembely zaidi ya uwanja wao wa nyumbani wa Liberty Stadium.

Amesema kiujumla kikosi chake kilikua na matarajio ya kucheza hatua ya fainali licha ya kupambana na upinzani mkali kutoka kwa Nottingham Forest ambao wamekubali kisago cha jumla ya mabao matatu kwa moja baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana wakiwa nyumbani juma lililopita.

Hii leo mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi daraja la kwanza nchini Uingereza inaendelea tena kwa kushuhudia mchezo kati ya Cardif City dhidi ya Reading utakaounguruma kwenye uwanja wa Cardiff City.

Meneja wa Cardif City Dave Jones ametamba kufanya vizuri katika mchezo huo kufuatia maandalizi safi aliyoyafanya akiwa na kikosi chake kwa muda wa juma moja lililopita.

Nae meneja wa klabu ya Reading Brian MCDERMOTT amethibitisha uwepo wa ari ya ushindi katika kikosi chake hivyo anaamini mambo yatakua mazuri baada ya dakika 90 za mchezo huo wa soka.

Mshindi kati ya Cardiff City dhidi ya Reading atapambana na Swansea katika mchezo wa hatua ya fainali utakaochezwa May 30 kwenye uwanja wa Wimbely kwa ajili ya kumpata mshindi atakaepanda daraja na kucheza ligi kuu ya nchini Uingereza msimu ujao.

Tayari klabu za Norwich City pamoja na QPR zimeshafanikiwa kupanda daraja baada ya kumaliza katika nafasi mbili za juu katika msimamo wa ligi daraja la kwanza msimu huu.

No comments:

Post a Comment