KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 31, 2011

Carles Puyol KUPASULIWA KESHO.


Nahodha na beki wa klabu bingwa nchini Hispania pamoja na barani Ulaya kwa ujumla FC Barcelona Carles Puyol kesho anatarajia kufanyiwa upasuaji wa goti.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 33 atafanyiwa upasuaji huo na madaktari wawili Ricard Pruna pamoja na Ramon Cugat huku ikiaminiwa kwamba atarejea katika hali yake ya kawaida kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Kufuatia hatua hiyo Carles Puyol amelazimika kuachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania ambacho kinajiandaa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Marekani pamoja na Venezuela mapema mwezi ujao.

Pia imeelezawa kwamba matatizo hayo ya goti yalichangia kutokujumuishwa kwenye kikosi kilichoanza mchezo wa hatua ya fainali ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Man utd waliokubali kibano cha mabao matatu kwa moja, na badala yake alipatiwa nafasi katika dakika za mwishoni za mchezo huo baada ya kutolewa kwa Daniel Alves.

No comments:

Post a Comment