KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 20, 2011

CARLOS TEVEZ AENDA KINYUME NA KAULI YA BOSI WAKE.


Siku mbili baada ya meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini kuthibitisha taarifa za mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez kuendelea kuwepo klabuni hapo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi hii leo mshambuliaji huyo ameibuka na kukanusha taarifa hizo.

Carlos Tevez amekanusha taarifa hizo huku akieleza wazi dhamira yake ya kutaka kuondoka katika himaya ya klabu hiyo yenye mskani yake makubwa huko mjini Manchester nchini Uingereza.

Akihojiwa na kituo cha Radio del Plata cha nchini kwao Argentina mshambuliaji huyo amesema umewadia wakati sasa kwa yeye binafsi kusaka mafanikio zaidi nje ya klabu ya Man City ambayo amekiri imefunda vya kutosha hali iliyopelekea kucheza kwa kujituma wakati wote.

Teves mwenye umri wa miaka 27 amesema lengo lake kubwa ni kutaka kutimiza ndoto yake ya kucheza katika vilabu zaidi ya vitatui na kuvipa mafanikio kama ilivyokuwa kwa West ham utd ambao aliwapigania hadi kusalimika kutokushuka daraja msimu wa mwaka 2006-07, kisha akaelekea Man Utd ambapo huko alifanikiwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliotwaa ubingwa wa ligi katika msimu wa mwaka 2007–08 na 2008–09, ngao ya hisani katika msimu wa mwaka 2008-09, ubingwa wa kombe la ligi *Curling CUP* katika msimu wa mwaka 2008–09, ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya katika msimu wa mwaka 2007–08 pamoja na ubingwa wa klabu bingwa duniani mwaka 2008.

Tayari klabu ya Inter Milan pamoja na Juventus zote za nchini Italia zimeshaanza kuhusishwa na taarifa za kutaka kumsajili Carlos Tevez kwa ajili ya msimu ujao wa ligi lakini pia zipo taarifa nyingine zinazobainisha kwamba huenda mshambuliaji huyo akaamua kurejea nyumbani kwao Argentina na kujiunga na klabu yake ya zamani ya Boca Junior.

Kama itakumbukwa vyema meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini alitoa kauli ya uthibitisho wa kubaki kwa mshambuliaji huyo huko City Of Manchester katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Stoke City ambao walikuabali kisago cha mabao matatu kwa sifuri.

No comments:

Post a Comment