KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 25, 2011

David De Gea NDIE MRITHI WA Edwin van der Sar.


Kipa wa kimataifa toka nchini Hispania pamoja na klabu ya Atletico Madrid David De Gea yu mbioni kujiunga na mabingwa wa soka nchini Uingereza Manchester United kwa lengo la kuziba nafasi inayoachwa wazi na Edwin van der Sar.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 21 anajipanga kuelekea Old Trafford, kufuatia uwezo wake kuonekana mkubwa huku ikiaminiwa ana kila sababu za kuziba nafasi ya Edwin van der Sar ambae atatundika Gloves mara baada ya mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Fc Barcelona utakaochezwa mwishoni mwa juma hili huko jijini London.

Meneja wa Man Utd Sir Alex Ferguson usiku wa kuamkia hii leo alithibitisha taarifa za kipa huyo kuwa mbioni kujiunga na kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi huku akieleza wazi kwamba David De Gea ana sifa zote anazozihitaji.

Thamani ya kipa huyo ni kiasi cha paund million 18 ambacho kimetajwa na uongozi wa klabu ya Atletico Madrid kama ada ya uhamisho wake kutoka nchini Hispania.

No comments:

Post a Comment