KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 17, 2011

Diego Armando Maradona KUFUNDISHA SOKA UARABUNI.


Gwiji wa soka nchini Argentina Diego Armando Maradona amerejea tena katika tasnia ya mchezo huo kufuatia kuteuliwa kuwa meneja wa klabu ya Al Wasl iliyo na maskani yake makuu huko falme za kiarabu.

Diego Armando Maradona anarejea katika tasnia ya mchezo wa soka baada ya kuenguliwa katika nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Argentina mara baada ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 zilizochezwa huko nchini Afrika kusini.

Taarifa zilizothibitishwa na mwenyekiti wa klabu ya Al Wasl Marwan Bin Bayat zimeeleza kwamba tayari wameshakamilisha taratibu zote na Diego Armando Maradona na kwa sasa wanachosubiri ni hatua ya meneja huyo kuanza kazi yake rasmi.

Marwan Bin Bayat pia akasisitiza suala la kuamini kwamba uwepo wa Maradona katika klabu yao utawawezesha kufanya vizuri katika ligi ya nchi za falme za kiarabu ambapo kwa sasa kikosi chao kinakamata nafasi ya nne katika msimamo wa ligi.

No comments:

Post a Comment