KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 20, 2011

Edinson Cavani


Hatimae mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uruguay pamoja na klabu ya Napoli Edinson Cavani amekata ngebe za waandishi wa habari wa nchini humo pamoja na wale wa nchini Uingereza ambao siku za nyuma walikua wakiripoti yu mbioni kuihama klabu hiyo.

Edinson Cavani amekata ngebe za waandishi wa habari kufuatia maamuzi yake ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Napoli kwa muda wa miaka mitano ijayo, huku sababu kubwa ya kufanya hivyo ikitajwa ni kupatikana kwa nafasi ya klabu hiyo kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambae msimu huu amekua chachu ya kupatikana kwa mafanikio huko Stadio San Paolo tayari alikua anahusishwa na taarifa za kuwa mbioni kusajiliwa na klabu za Manchester City, Chelsea, Tottenham pamoja na Real Madrid.

Mwenyekiti wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis usiku wa kuamkia hii leo alijitokeza hadharani kupitia kituo cha televisheni kinachomilikiwa na klabu hiyo na kutoa uthibitisho wa taarifa za kumsainisha mkataba mpya Edinson Cavani.

No comments:

Post a Comment