KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, May 21, 2011

Emmanuel Adebayor AJIPIGIA UPATU KUBAKI MADRID.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Togo Emmanuel Adebayor bado anaamini huenda uongozi wa klabu hiyo ukamsajili moja kwa moja baada ya kumsajili kwa mkopo akitokea Man City mwezi januari mwaka huu.

Emmanuel Adebayor ameonyesha kuwa na imani hiyo alipohojiwa na kituo kimoja cha televisheni cha mjini Madrid ambapo amekiri anaipenda klabu hiyo na tayari ameshatengeneza mazingira mazuri ya kuwa na marafiki wa kila aina mjini humo kufuatia uwezo wake anapokua uwanjani.

Toka alipojiunga na Real Madrid mwezi Januari, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amecheza michezo 21 na kupachika mabao matano.

No comments:

Post a Comment