KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 30, 2011

FIFA HALI SI SHWARI.

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetangaza kuwasimamisha kwa muda wajumbe wawili wa kamati kuu ambao ni Mohamed Bin Hammam pamoja na Jack Warner kufuatia uchunguzi wa tuhuma za rushwa kubaini walihusika na tuhuma hizo wakiwa katika mikakati ya kuomba kura za uraisi.

FIFA wametangaza maamuzi hayo kupitia kamati ya maadili ambayo jana ilifanya mahojiano na watuhumiwa hao kwa lengo la kutafuata ukweli wa jambo hilo ambalo limekua likipigwa vita kubwa.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Petrus Damaseb alitangaza maamuzi ya kamati hiyo kwa kusema kwamba watuhumiwa hao wana kesi ya kujibu kufuatia tuhuma zinazowakabili za kutoa mlungula kwa wajumbe wa shirikisho la soka la Caribbean ili waweze kumpigia kura Mohamed Bin Hammam ambae alikua anawania nafasi ya uraisi wa FIFA kabla ya kutanmgaza kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho usiku wa kuamkia jana.

Maafisa wengine wawili wa FIFA pia wamesimamishwa ambao ni Debbie Minguell na Jason Sylvester baada ya kubainika walihusika na tuhuma hizo.

Katika hatua nyingine Jopes Sepp Blatter raisi wa sasa wa FIFA amewashiwa taa za kijani kwa ajili ya kuendelea na kampeni zake za kutetea kiti cha uraisi baada ya kuonekana hana kesi ya kujibu katika sakata hilo.

Blatter nae alihojiwa kuhusiana na sakata hilo ambapo inadaiwa alifahamu kilichokua kikiendelea kati ya wajumbe wa Caribian dhidi ya Mohamed Bin Hammam na Jack Warner lakini alikaa kimya.

Katibu mkuu wa FIFA Jorome Valke ametangaza utaratibu wa kuendelea kwa Blatter katika harakati zake za kuomba kura.

No comments:

Post a Comment