KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 24, 2011

FIFA WAENDELEA KUSAKA DAWA YA KUJISAFISHA.


Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA bado linaendelea kusaka ushahidi wa sakata la rushwa linalowakabili baadhi ya wajumbe wa shirikisho hiloa mbao wanadaiwa kuhusika na sakata hilo wakati wa kusaka wenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 pamoja na 2012.

Uthibitisho wa kufanyika kwa harakati hizoumetolewa na raisi wa FIFA Josep Sepp Blatter akiwa nchini Japan alipokwenda katika ziara ya kujipigia upatu wa kuomba kura.

Amesema kwa hivi sasa wamekua na mawasiliano mazuri na wahusika wa gazeti la Sunday Times la nchini Uingereza kw alengo la kupatiwa ushahidi ili waweze kutimiza zogo hilo lililoibuliwa na mwenyekiti wa zamani wa chama cha soka nchini Uingereza David Triesman.

Mbali na kuwepo kwa uataratibu huo FIFA bado wameendelea kumtaka David Triesman kuwasilisha uthibitisho utakaothibitisha ukweli wa jambo alilolizungumza katika bunge la nchini Uingereza alipokwenda kujieleza kwa nini Uingereza ilikosa nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia.

Wakati huo huo Blatter amesema katika upande wa michuano ya klabu bingwa duniani ambayo ipi chini ya shirikisho hilo kila kitu kipo vizuri kwa hivi sasa na michuano hiyo imepangwa kufanyika nchini japan mwezi Disemba mwaka huu.

Amesema sababu kubwa ya kuchaguliwa kwa nchi hiyo kuhodhi michuano hiyo ni kutaka kutoa mkono wa pole kwa mashabiki wa soka nchini humo kufuatia janga la sunami lililojitokeza mapema mwaka huu nchini Japan.

No comments:

Post a Comment