KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 20, 2011

FRED ARUDISHWA KUNDINI.


Nahodha na mshambuliaji wa klabu ya Fluminense Frederico Chaves Guedes *Fred*, amerejeshwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil baada ya kuitwa na kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Mano Menezes.

Frederico Chaves Guedes amerejeshwa kikosini baada ya miaka minne kuwa nje ya kikosi hicho ambapo kwa mara ya mwisho aliitumikiwa timu ya taifa ya Brazil mwaka 2007 kwenye fainali za mataifa ya Amerika ya kusini *Copa America*.

Kuitwa kwake katika kipindi hiki kunatokana na uwezo mkubwa anaouonyesha akiwa na klabu yake ya Fluminense, ambayo imekua ikifanya vyema katika michezo ya ligi ya nchini Brazil ambayo msimu uliopita ilikishuhudia kikosi cha klabu hiyo kikiibuka mabingwa.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil ameita kikosi cha wachezaji 28 huku akimuacha kiungo wa klabu ya Real Madrid Ricardo Izecson dos Santos Leite kaka, pamoja na kiungo wa klabu ya Flamengo Ronaldo de Assis Moreira Ronaldinho Gaucho kwa ajili ya michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi pamoja na Romania itakayochezwa mwezi ujao.

Kaka ameachwa kikosini kufuatia kuhitaji muda wa kupumzika baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu kwa sababu za kuwa mejeruhi wa muda mrefu lakini Ronaldinho amachwa kwa sababu za uwezo wake kuporomoka mbali na ilivyokua siku za nyuma.

Kikosi kamili cha timu ya taifa ya Brazil kilichoitwa kwa ajili ya michezo hiyo miwili ya kimataifa ya kirafiki ambayo itaijenga timu hiyo kabla ya fainali za mataifa ya Amerika ya kusini zitakazochezwa nchini Argentina kuanzia July 1–July 24.

Upande wa makipa:

Victor (Gremio), Jefferson (Botafogo), Julio Cesar (Inter Milan), Fabio (Cruzeiro)

Mabeki: Lucio, Maicon (both Inter Milan), Thiago Silva (AC Milan), David Luiz (Chelsea), Luisao (Benfica), Andre Santos (Fenerbahce), Daniel Alves, Adriano (both Barcelona)

Viungo: Lucas (Sao Paulo), Lucas Leiva (Liverpool), Elano (Santos), Elias (Atletico Madrid), Henrique (Cruzeiro), Jadson (Shakhtar Donetsk), Ramires (Chelsea), Sandro (Tottenham Hotspur), Thiago Neves (Flamengo), Anderson (Manchester United)

Washambuliaji: Alexandre Pato, Robinho (both AC Milan), Neymar (Santos), Nilmar (Villarreal), Fred (Fluminense), Leandro Damiao (Internacional)

No comments:

Post a Comment