KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 27, 2011

Gervais Yao Kouassi Gervinho AWINDWA NA RADA ZA KIINGEREZA.


Mshambulaiji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast pamoja na klabu bingwa nchini Ufaransa Lille, Gervais Yao Kouassi Gervinho amesema yu tayari kufanya maamuzi yatakayoamua mustakabali wa maisha yake ya soka katika msimu ujao.

Gervinho, mwenye umri wa miaka 23, ametoa msisitizo huo wa maamuzi kufuatia klabu ya Arsenal, Liverpool pamoja na Newcastle kuhusishwa na taarifa za kutaka kumsajili baada ya kuvutiwa na uwezo wake ambao ulichangiwa kwa kiasi kikubwa kuisaidia klabu ya Lille kutwaa ubingwa wa nchini Ufaransa msimu wa mwaka 2010-11.

Amesema maamuzi ya kuihama klabu yake ya nchini Ufaransa ama kubaki atayatoa mara baada ya mchezo wa kimataifa ambao utashuhudia timu ya taifa ya Ivory Coast ikiendelea na kampeni za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2012 kwa kucheza na timu ya taifa ya Benin mwanzoni mwa mwezi ujao.

Hata hivyo amedai kwamba meneja wa klabu ya Lille Rudi Garcia amemtaka kubaki klabuni hapo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

No comments:

Post a Comment