KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 27, 2011

HATOTOWAIGA WANAVYOCHEZA HATA KIDOGO.


Beki wa kimataifa toka nchini Serbia pamoja na klabu bingwa nchini Uingereza Man Utd Nemanja Vidic amesema hawana budi kucheza mchezo wao hiyo kesho katika mpambano wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Fc Barcelona.

Vidic amesema anaamini siri kubwa ya kuwashinda kirahisi FC Barcelona katika mchezo huo ni kuhakikisha wanatumia nafasi ya kuenzi mfumo wao wakati wote na si kuiga mfumo wa mabingwa hao wa nchini Hispania ambao hupenda kutumia pasi fupi fupi.

Amesema hakuna linaloshindikana katika mchezo huo hasa ikizingatiwa tayari wameshapata muda wa kutosha wa kujiandaa na mchezo huo ambao ana hakika hautotoa nafasi kwa kwa wapinzani kuipenya ngome yao ya ulinzi kirahisi.

Hata hivyo amedai kwamba yeye binafsi yu tayari kupambana wakati wote na anaamini ubingwa wa michuano hiyo utaelekea old Trafford na si Camp Nou kama ilivyokua katika fainali ya mwaka 2009 ambapo Barcelona waliibamiza Man utd mabao mawili kwa sifuri.

Sir Alexander Chapman "Alex" Ferguson meneja wa klabu ya Man Utd yeye amekiri wapinznai wao msimu huu wapo kivingine na si kama walivyopambana nao katika mchezo wa hatua ya fainali uliochezwa Stadio olympico mjini Roma nchini Italia mwaka 2009.

Ferguson amekiri kuwepo kwa mabadiliko hayo alipokua akijibu swali la mmoja wa waandishi wa habari ambae alitaka kufahamu namna babu huyo anavyowaona wapinzani wao ambao wametinga katika hatua ya fainali baada ya kuwabanjua Real Madrid.

Josep Pep Guardiola Isala, nae amekiri kuendelea kushangazwa na nguvu ya ajabu iliopo katika kikosi cha Man Utd ambacho kimekua hakiwategemei baadhi ya wachezaji kama ilivyo katika klabu nyingine.

Amesema alikwenda katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali uliochezwa huko Old Trafford ambapo wenyeji Man Utd walicheza na Schalke 04 na kikubwa alichokiona ni mabadiliko ya wachezaji tisa na timu ilicheza vizuri hivyo hana budi kukubali na kuuheshimu mfumo wa Sir Alex Ferguson .

No comments:

Post a Comment