KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 30, 2011

HOFU YATANDA KATIKA KAMBI YA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini ujerumani pamoja na klabu ya Bayern Munich Miroslav Klose amejiondoa katika timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo itarejea katika kamepni za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya za mwaka 2012 kwa kupambana na Austria pamoja na Azerbaijan mapema mwezi ujao.

Miroslav Klose amejiondoa kikosini kufuatia maumivu makali ya mbavu yanayomkabili baada ya kuumia akiwa katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa jana dhidi ya timu ya taifa ya Uruguay ambayo ilikubali kisago cha mabao mawili kwa moja.

Kabla ya kupata maumivu ya mbavu Miroslav Klose alifanikiwa kuifungia Ujerumani bao la kuongoza katika dakika ya 20 kabla ya André Schürrle hajapachika bao la pili na la ushindi katika daklika ya 35 huku Walter Gargano akifunga bao la kufutia mchozi kwa upande wa Uruguay katika dakika ya 48.

Kuumia kwa mshambuliaji huyo mwenye Klose 32 kunatoa nafasi kwa mshambuliaji mwenzake wa klabu ya Bayern Munich Mario Gomez kuanza kufikiriwa kuitumikia nafasi hiyo hatua mbayo ilianza kutimizwa katika mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki.

Ujerumani wanatarajia kurejea kwenye kampeni ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Ulaya za mwaka 2012 huku wakiwa wanaongoza kundi lao kwa tofauti ya point tano na mchezo ujao unatarajiwa kucheza June 3 dhidi ya Austria na kisha siku tatu baadae timu hiyo itacheza na Azerbaijan.

No comments:

Post a Comment