KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 17, 2011

INTER MILAN YATANGAZA DAU KWA Eden Hazard.


Waliokua mabingwa nchini Italia Internazionale wapo katika harakati nzito za kuanza kujiimarisha katika suala la kufanya usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Inter Milan wapo katika harakati hizo huku jicho lao kwa sasa likimtazama vilivyo kiungo wa kimataifa toka nchini Ubelgiji pamoja na klabu inayotarajiwa kutwaa ubingwa wa nchini Ufaransa LILLe Eden Hazard.

Tayari uongozi wa klabu hiyo ya nchini Italia umeshatangaza kutenga kiasi cha paund million 20 ambacho kinadhaniwa huenda kikatosha katika utaratibu wa uhamisho wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20.

Raisi wa Inter Milan Massimo Moratti amepata jeuri ya kutaka kumsajili kiungo huyo kufuatia kauli aliyoitoa siku za hivi karibuni ambayo ilieleza kwamba anatamani kucheza katika klabu kubwa barani ulaya sambamba na kubadili mazingira ya soka lake.

Eden Hazard mpaka sasa ameshaitumikiwa Lille michezo 106 na kufunga mabao 16.

No comments:

Post a Comment