KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 30, 2011

Jack Warner AMWAGA SIRI HADHARANI !!


Makamu wa rais wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA, Jack Warner, ametoboa siri kwa kuonyesha hadharani barua pepe ambayo inadai Mohamed Bin Hammam alinunua kura ambazo ziliiwezesha nchi yake ya Qatar kushinda nafasi ya kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022.

Jack Warner amefanya hivyo kwa kuwaonyesha waandishi wa habari barua hiyo ikiwa ni sehemu ya kutaka kujitetea na tatizo linalomkabili kwa sasa ambalo limepelekea kusimamishwa kwa muda na kamati ya maadili iliyokutana jana na kuafiki maamuzi hayo.Kiongozi huyo amedai kwamba bado kuna baadhi ya watu ndani ya FIFA wanahusika kuchukua mlungula na si yeye pekee yake huku akimuhusisha katibu mkuu Jerome Valcke ambae anadaiwa alipata taarifa hizo kupitia barua pepe ambayo ilionyesha majina ya Josep Sepp Blatter pamoja na Mohamed Bin Hammam kwa kifupi.

Katika barua hiyo ujumbe wa Valcke unasomeka kwamba Bin Hammam anadhani unaweza kuinunua FIFA kama alivyonunua fainali za Kombe la Dunia.

Hata hivyo katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke amekiri alipokea barua hiyo kwa njia ya mtandao wa Internet kutoka kwa Jack Warner, ambae alikua anahoji kigezo kilichotumika kumruhusu Bin Hammam kuwania nafasi ya uraisi ili hali anahusika na uchafu huo alioufanya?

Katika utetezi wake mbele ya waandishi wa habari Valcke ameeleza kwamba barua hiyo ilikua ni ya kibinafsi na si ya kiofisi na bado Jack Warner alikuwa amehusika katika sehemu ya barua hiyo.
Valcke pia amekanusha taarifa za kuishurutisha kamati ya maadili ya FIFA ambayo imemsimamisha kwa muda Jack Warner pamoja na na Bin Hammam kufuatia tuhuma zinazowakabili za kutoa mlungula kwa wajumbe wa CONCACAF kwa ajili ya kumpgia kura Bin Hammam katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika June mosi mjini Zurich nchini Uswiz.

Maamuzi ya kusimamishwa kwa watuhumiwa hao wawili yalitangazwa jana na makamu mwenyekiti wa kamati ya maadili ya FIFA Petrus Damaseb.

Katika hatua nyingine Jopes Sepp Blatter raisi wa sasa wa FIFA amewashiwa taa za kijani kwa ajili ya kuendelea na kampeni zake za kutetea kiti cha uraisi baada ya kuonekana hana kesi ya kujibu katika sakata hilo.

Blatter nae alihojiwa kuhusiana na sakata hilo ambapo inadaiwa alifahamu kilichokua kikiendelea kati ya wajumbe wa Caribian dhidi ya Mohamed Bin Hammam na Jack Warner lakini alikaa kimya.
Kufuatia hatua hiyo Katibu mkuu wa FIFA Jorome Valke ametangaza utaratibu wa kuendelea kwa uchaguzi mkuu kama ulivyokua umepangwa siku za nyuma.

Na taarifa tulizozipata hivi punde zinaeleza kwamba raisi wa shirikisho la soka barani Asia Mohamed bin Hammam anatarajia kukata rufaa kufuati maamuzi ya kusimamishwa kwake na kamati ya maadili ya shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA.

Mohamed bin Hammam anatarajiwa kuwasilisha rufaa yake katika kamati ya rufaa ya FIFA siku yoyote ndani ya juma hili huku akiamini kwamba bado ana haki kufuatia tuhuma zinazomkabili za utoaji wa rushwa ambao umetajwa kufanyika katika kamepni zake huko Amerika ya kati.

Wakati huo huo shirikisho la soka nchini Qatar limekanusha vikali taarifa zilizotolewa makamu wa raisi wa FIFA aliesimamishwa Jack Warner ambazo zimedai kwamba nchi hiyo ilimtumia mlungula ili iweze kuibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022.

No comments:

Post a Comment