KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 30, 2011

Javier Aguirre AKUBALI KUSAINI MKATABA MPYA.


Meneja wa klabu ya Real Zaragoza Javier Aguirre amekubali kuongeza mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi cha klabu hiyo ambacho kimenusurika kushuka daraja katika msimu wa mwaka 2010-11.

Javier Aguirre ambae liiongoza timu ya taifa ya Mexico katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 zilizofanyika nchini Afrika kusini amefanya maamuzi ya kuendelea kubaki huko La Romareda, baada ya makubaliano yaliyofikiwa katika vikao ambavyo vilimshirikisha yeye binafsi pamoja na uongozi wa klabu hiyo.

Sababu kubwa ya meneja huyo mwenye umri wa miaka 52 kuombwa kuendelea kufanya shughuli ya kukiongoza kikosi cha Real Zaragoza ni ufabnisi wake mkubwa aliouonyesha toka alipopewa jukumu hilo mwezi Novemba mwaka jana baada ya kutimuliwa kazi kwa Jose Aurelio Gay.

Real Zaragoza walinusurika kushuka daraja katika msimu wa mwaka 2010-11 katika mchezo wao wa mwisho wa LA LIGA dhidi ya Levante ambao walikubali kisago cha mabao mawili kwa moja.

No comments:

Post a Comment