KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 19, 2011

Jermain Defoe ACHOSHWA NA UTARATIBU WA BABU.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza pamoja na klabu ya Tottenham Hotspurs Jermain Defoe amesema hana raha ndani ya klabu hiyo kufuatia hatua ya kuenguliwa katika kikosi cha kwanza cha Harry Redknapp.

Jermain Defoe amesema hatua hiyo inamkera kwani lengo lake kila kukicha ni kutaka kucheza kila mchezo tena kwa kushirikishwa katika kikosi cha kwanza na hatua hiyo inampa changamoto kufuatia kiwango chake kuwa kizuri mazoezini hata anapopewa nafasi kwa muda mchache uwanjani.

Amesema lengo lake kubwa ni kutaka kuisaidia spurs kufikia melengo yaliyowekwa huko White Hart Lane kama ilivyokua msimu uliopita ambapo alisaidiana na wengine kuifikisha klabu hiyo katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Jermain Defoe alilazimika kurejeshwa tena Spurs mwaka 2009 baada ya kuajiriwa kazi kwa meneja Harry Redknapp ambae alimsajili katika utawala wake ndani ya klabu ya Portsmouth mwaka 2008 akitokea jijini London.

Kurejea kwake huko White Hart Lane pia kulisababishwa na hatua ya kuendelea kuwepo katika mipango ya Harry Redknapp, lakini toka mwanzoni mwa msimu huu mshambuliaji huyo amekua akikalishwa benchi na kusubiri kuchukua nafasi za wachezaji wengine.

No comments:

Post a Comment