KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, May 21, 2011

Jerzy Dudek KUWAAGA MASHABIKI HII LEO


Kipa wa kimataifa toka nchini Poland Jerzy Dudek hii leo atacheza mchezo wa mwisho akiwa na klabu yake ya Real Madrid ambayo msimu huu imeshindwa kutimiza malengo kuwapokonya ubingwa mahasimu wao wakubwa Fc Barcelona.

Jerzy Dudek atajumuika na wachezaji wenzake ikiwa ni sehemu ya kuwaaga mashabiki wa klabu ya Real Madrid huko Estadio Stantiago Bernabeu alipodumu kwa muda wa miaka minne iliyopita baada ya kuachana na klabu yake ya zamani wa Liverpool ya nchini Uingereza.

Uongozi wa klabu ay Real Madrid tayari umeshampa heshima za mwisho kipa huyo mwenye umri wa miaka 38 kwa kumfanyia tafrija ya kumuaga sambamba na wachezaji wenzake atakaowaacha klabuni hapo na hii imekuja kufuatia mkataba wake kufikia kikomo mwishoni mwa msuimu huu.

Jerzy Dudek toka alipofika huko Estadio Stantiago Bernabeu mwaka 2007 amekua na wakati mgumu wa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid kufuatia uwepo wa kipa nambari moja Iker Casillas ambae pia ni chaguo la kwanza kwenye timu ya taifa ya Hispania.

Dudek, ambae ameitumikia timu ya taifa ya Poland michezo 59 anaondoka Real Madrid huku akiweka kumbukumbu nzuri ya kuwa miongoni mwa wachezaji walioweza kutwaa ubingwa wa ligi ya nchini Hispania mwaka 2008 na pia ubingwa wa kombe la mfalme mwezi uliopita.

Real Madrid hii leo wanafunga msimu wa ligi ya nchini Hispania kwa kucheza na klabu ya Almeria.

No comments:

Post a Comment