KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 31, 2011

Josep Sepp Blatter AKANUSHA FIFA KUYUMBA.


Rais wa shirikisho la Soka ulimwenguni kote FIFA Josep Sepp Blatter amekanusha taarifa za shirikisho hilo kuwa katika hali ya msukosuko kufuatia kashfa za rushwa zinazo waandama baadhi ya wajumbe wa kamati kuu.

Blatter amekanusha taarifa hizo alipozungumza na waandishi wa habari huko mjini Zurich nchini Uswiz ambapo amesema hakuna hali hiyo na aamini kilichopo ni matatiozo madogo madogo ambayo yanaweza kutatuliwa na watu wa FIFA wenyewe.

Amesema FIFA inaendeshwa kwa misingi ya katiba ilopo na kila mmoja wao anastahili kufuata utaratibu huo na anaamini hali hiyo itasaidia kumaliza matatizo madogo madogo yanayowakabili kwa sasa.

Hata hivyo Josep Sepp Blatter hakumaliza mkutano huo na waandishi wa habari kwa usalama, kufuatia majibizano yaliyojitokeza kati yake na waandishi wa habari wa nchini Ujerumani ambao walitaka kujua nini msimamo wake wa kuendelea kuwa raisi wa FIFA ili hali kuna kashfa nzito inayowakabili kwa sasa.

Blatter alichowajibu waandihi hao ni kwamba anastahili kuheshimiwa hasa ikizingatiwa nae alikua muandishi wa habari na sifa kubwa ya kuwa katika kazi hiyo ni kuhakikisha suala la nidhamu linazingatiwa.

Utaratribu huo wa Blatter wa kuzungumza na waandishi wa habari bado ulionekana kushangaza pale alipoingia katika chumba cha mikutano akiwa pekee yake hatua ambayo si ya kawaida kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment