KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 26, 2011

KIKOSI CHA AFRIKA CHAANGUKIA KIDEVU.


Kikosi maalum cha dunia kilichoundwa na wachezaji 11 kimefanikiwa kukifunga kikosi maalum cha Afrika kilichokua kikiongozwa na kiungo wa kimataifa toka nchini Ghana pamoja na klabu ya chelsea Michael Kojo Essien katika mchezo wa kuhimiza suala la amani barani Afrika.

Mchezo huo ambao ulichezwa jana mjini Accra nchini Ghana ambao pia ulichukua sehemu ya kusheherekea siku ya Afrika ulishuhudia kikosi cha dunia kikikichabanga kikosi cha barani Afrika mabao manne kwa mawili.

Mabao kwa upande wa timu ya wachezaji wa barani Afrika yalipachikwa na gwiji wa soka toka nchini Zambia Kalusha Bwalya pamoja na nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba huku mabao ya kikosi cha timu ya wachezaji wa dunia yakipachikwa nyavuni na Scott Smith, Yaw Preko, Florent Malouda pamoja na Ashley Cole.

Kikosi cha kilichounda timu ya dunia kiliwahusisha wachezaji kama:
Nick Hamman-Lockwood Matt, Nigel de Jong, Freddie Ljungberg, Yaw Preko, Ellis Tebbunt, Quincy Owusu Abeyie, Jalloh Musa Akeem, Ashley Cole, Florenet Malouda pamoja na Scott Smith.

Kikosi cha kilichounda timu ya Africa kiliwahusishwa wachezaji kama:
Richard Kinsgon, Nkwankwo Kanu, Stephen Appiah, Kalusha Bwalya, Sammy Kuffour, Michael Essien, Asamoah Gyan, John Painstil, Salomon Kalou, Rabah Madjer pamoja na Yakubu Aiyegbeni.

No comments:

Post a Comment