KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 27, 2011

KOLO TOURE JELA MIEZI SITA !!!!


Hatimae suala la beki wa kimataifa toka nchini Ivory Coast pamoja na klabu ya Manchester City Habib Kolo Toure la kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni, limefikia tamati kwa mchezaji huyo kuingizwa katika jela ya soka.

Hukumu ya Habib Kolo Toure imesomwa na kamati ya nidhamu ya chama cha soka nchini Uingereza FA ambapo mchezaji huyo atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita.

Maamuzi hayo yanamaanisha wazi kwamba beki huyo mwenye umri wa miaka 30 atarejea tena katika shughuli za mchezo wa soka mapema mwezi wa tisa ambapo hukumu hiyo imeanza kuhesabiwa toka March mbili siku ambayo iliyothibitika anatumia dawa za kuongeza nguvu baada ya kufanyiwa vipimo.

Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ambae alipata nafasi ya kumlea Habib Kolo Toure kuanzia mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 21, aliziungumzia masikitiko yake baada ya mchezaji huyo kubainika anatumia dawa za kuongeza nguvu michezoni.

Hata hivyo Wenger alisema baada ya kusikia taarifa hizo alizungumza na Kolo Toure na kumuuza kulikoni? Ambapo alimjibu alitumia dawa za mke wake za kupunguza uzito na kwa habati mbaya alipofanyiwa vipimo alikutwa na chembe chembe za dawa hizo ambazo zinafanya kazi nyingine ya kuongeza nguvu mwilini.

No comments:

Post a Comment