KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 25, 2011

KURA NITAMPA MMOJA WAO LAKINI KWA AHADI ZA UKWELI.


Matumaini ya raisi wa sasa wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Josep Sepp Blatter ya kupata kura zote za barani Afrika yameendelea kufifia kufuatia raisi wa shirikisho la soka nchini Rwanda (FERWAFA) Jean Bosco Kazura kumtaka raisi huyo pamoja na mpinzani wake Mohammed Bin Hammam kueleza wazi wataisaidia vipi nchi hiyo endapo wataingai madarakani.

Jean Bosco Kazura amehoji suala hilo huku zikiwa zimesalia siku sita kabla ya hatua ya upogaji wa kura halijachukua nafasi yake huko mjini Zurich nchini Uswiz huku kamati kuu ya shirikisho la soka barani Afrika CAF ikiwa tayari imeshamthibitishia Blatter kupata kura zote kutoba barani humo.

Raisi huyo wa (FERWAFA) amesema kuna ulazima kwa wagombe hao kueleza mikakati yao ya kuisaidia nchi ya Rwanda kabla hawajachukua maamuzi ya kumpigia kura mmoja wao ili ifahamike wazi kwamba FIFA wana mpango gani na soka la nchini humo.

Mbali na Rwanda Jean Bosco Kazura akageukia maendeleo ya soka la barani Afrika ambayo yanakwenda kwa kusua sua kila siku zinazorejea kwa mwenyezi mungu ambapo amesema si mara ya kwanza kwa viongozi wa FIFA kuja barani humo na kuomba kura na kisha wanapomalizia shida zao husahau namna ya kutoa misaada ya kuendeleza mchezo wa soka.

Mohamed Bin Hammam anaewania kiti cha uraisi wa FIFa akitokea nchini Qatar katika bara la Asia, mwezi uliopita alizulu nchini Rwanda na kufanya mkutano na makamu wa raisi wa nchi hiyo Bernard Makuza kwa lengo la kumtaka kuwashawishi viongozi wa (FERWAFA) kumpigia kura.

Mohamed Bin Hammam anawani kiti cha uraisi wa FIFA dhidi ya Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 75 ambae pia amekua madarakani toka mwaka 1998.

No comments:

Post a Comment