KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 23, 2011

Manuel Neuer BADO YU NJIA PANDA.


Kipa wa kimataifa toka nchini Ujerumani Manuel Neuer huenda akasalia katika hima Veltins-Arena, huko Gelsenkirchen kufuatia mpango wake wa kutaka kujiunga na klabu ya Bayern Munich kusua sua.

Mwenyekiti wa klabu ya Schalke Clemens Toennies amesema mazungumzo kati yao na viongozi wa Bayern Munich yamekua katika mazingira magumu kufuatia suala la fedha ambayo imeshaanikwa hadharani kama ada ya uhamisho wa kipa huyo.

Ada ya uhamisho wa kipa huyo ni paund million 20 na uongozi wa Bayern Munich umekua ukibembeleza kupunguziwa kiasi hicho hadi kufikia paund million 12.

Amesema kufuatia hatua hiyo wanafikiri kukaa chini na Manuel Neuer kwa ajili ya kuanza upya utaratibu wa kufanya nae mazungumzo ya kusaini mkataba mpya ambao utaendelea kumuweka huko Veltins-Arena.

Ikumbukwa kwamba Manuel Neuer tayari ameshagoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki klabuni hapo huku mkataba wake wa sasa na klabu ya Schalke ukitarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao, hivyo hatua ya uongozi wa klabu hiyo ya kutaka kukaa nae mezani itakua ikifanywa kwa mara ya pili.

No comments:

Post a Comment