KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 23, 2011

MASHABIKI WA MAN UTD WASHUKURIWA.


Mashabiki, wakereketwa na wafurukutwa wa klabu ya Man Utd wamepewa pongezi za shukurani kutoka kwa meneja wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson aliekiongoza kikosi chake kutwaa ubingwa wa 19 wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu wa mwaka 2010-11.

Pongezi za shukurani kwa mashabiki, wakereketwa na wafurukutwa wa Man utd zimetolewa na babu huyo wa nchini Scotland mara baada ya mchezo wa jana wa ligi ambapo mashetani wekundu walifanikiwa kupata ushindi wa mabao manne kwa mawili dhidi ya Blackpook ambao sasa wanarejea katika ligi daraja la kwanza.

Sir Alex Ferguson amesema ni faraja kubwa kuwa na mashabiki waliowapa nguvu wakati wote na kutoa faraja pale walipokwama hivyo kwa upande wake yeye aliona ni sehemu ya furaha na misukosuko waliyoipata katika msimu huu wa ligi ambao amekiri ulikua mgumu.


Edwin Van Der Sir kipa tegemezi wa klabu ya Man utd nae alipata nafasi ya kutoa shukurani zake za dhati kwa kila mmoja anaehusika na klabu hiyo huku akidai kwamba amekua na wakati mzuri sana huko old Trafford, pia alifurahishwa na uwepo wa upendo pamoja na mshikamano kutoka katika kila upande wa muhusika klabuni hapo hivyo kwa hatua hiyo alifarijika sana.

Edwin Van Der Sir alipata nafasi ya kuzungumza maneno hayo ikiwa ni sehemu yake ya mwisho ya kuwaaga mashabiki wa klabu ya Man Utd kufuatai maamuzi yake ya kutundika Gloves mara baada ya mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya utakaochezwa jijini London mwishoni mwa juma hili dhidi ya FC Barcelona.

No comments:

Post a Comment