KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 25, 2011

MECHI YA KUHIMIZA AMANI KUFANYIKA ACCRA-GHANA.


Wachezaji wa kiafrika wanaong’ara na vilabu vikubwa ulimwenguni wakiongozwa na kiungo wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza Michael Kojo Essien, wamewasili salama wa salmini huko nchini Ghana tayari kwa mchezo wa hisani utakaochezwa hii leo mjini Accra.

Wachezaji hao wamewasili mjini Accra toka jana wakitokea sehemu mbali mbali ulimwenguni sambamba na marafiki wanaocheza nao katika ligi za nje ya bara Afrika.
Essien ambae ndie kinara wa mchezo wa hii leo aliwasili mjini Accra akiwa sambamba na mshambuliaji pamoja na nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba, na Salomon Kalou huku wakiongozana na Ashley Cole wa nchini Uingereza pamoja na Florent Malouda wa nchini Ufaransa.

Wachezaji wengine waliowasili huko nchini Ghana tayari kwa mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa michezo wa Ohene Djan ni kiungo wa zamani wa klabu ya Arsenal pamoja na timu ya taifa ya Sweden Freddie Ljungberg, mchezaji bora wa dunia wa zamani kutoka barani Afrika George Oppong-Weah wa nchini Liberia pamoja na Emmanuel Adebayor wa nchini Togo.

Wachezaji wengine ni beki wa timu ya taifa ya Ghana John Painstil pamoja na winga Quincy Owusu-Abeyie walitarajiwa kuwasili mjini Accra hii leo, nahodha wa zamani wa kikosi cha Black Stars Stephen Appiah pamoja na beki wa kikosi cha vijana cha klabu ya Chelsea Daniel Pappoe.

Mchezo huo wa hisani kwa ajili ya kusheherekea siku ya Afrika utashuhudia kikosi cha wachezaji kumi na moja cha barani Afrika kikipambana na kikosi cha wachezaji 11 kutoka sehemu mbali mbali duniani.

No comments:

Post a Comment