KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 26, 2011

MTU MZIMA AKUBALIA KUBAKI SAN SIRO.


Hatimae kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi pamoja na klabu bingwa nchini humo Clarence Seedorf amekubali kusaini mkataba wa kuendelea kuitumikia Ac Milan yenye maskani yake makuu huko San Siro.

Clarence Seedorf amekubali kusaini mkataba huo baada ya kumbembelezwa toka juma lililopita ambapo ilikua inahofiwa huenda angeondoka klabuni hapo akiwa kama mchezaji huru mara baada ya kumalizika kwa msimu wa mwaka 2010-11.

Kiungo huyo mwenye umri wa mika 35 amekubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja ambao utafikia kikomo mwezi June mwaka 2012.

Hatua hiyo inaendelea kudhihirisha mipango ya uongozi wa klabu ya Ac Milan ya kuhakikisha wachezaji muhimu wanaendelea kubaki klabuni hapo kwa lengo la kusaidia utetezi wa ubingwa wa Sirie A walioutwaa msimu huu.

No comments:

Post a Comment