KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 17, 2011

MTU MZIMA Christoph Daum AJIVUA GAMBA.


Christoph Daum ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya umeneja wa klabu ya Eintracht Frankfurt kufuatia klabu hiyo kushindwa kujihakikishia kubaki katika ligi ya nchini humo kwa ajili ya msimu ujao.

Christoph Daum ametangaza maamuzi hayo usiku wa kuamkia hii leo baada ya kikosi cha Eintracht Frankfurt kukubalia kisago cha mabao matatu kwa moja kutoka kwa Borussia Dortmund mwishoni mwa juma lililopita.

Maamuzi ya meneja huyo mwenye umri wa miaka 57 yamekuja ikiwa ni miezi miwili na nusu toka alipoanza kuitumikia klabu hiyo ambayo ilifanikiwa kupata point mbili tu, kwenye michezo saba ambayo aliishuhudia katika utawala wake.

Katika taarifa yake aliyoitoa wakati wa kutangaza maamuzi ya kuachia ngazi usiku wa kuamkia hii leo Christoph Daum alisema uongozi wa klabu ya Frankfurt hauna budi kuanza upya utaratibu wa kurejea ligi kuu wakiwa na meneja mpya.

No comments:

Post a Comment