KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 24, 2011

MZOZO WA Olof Mattsson WANALIZWA Sierra Leone.


Kocha wa timu ya taifa ya Sierra Leone Olof Mattsson amesalimika katika harakati za kuendelea kukinoa kikosi cha taifa hilo ambacho kwa sasa kinasaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika zitakazochezwa mwaka 2012 katika nchi za Gabon pamoja na Equatorial Guinea.

Kusalimika kwa kocha huyo wa kimataifa toka nchini Sweden kunafuatia hatua ya kumalizika kwa malumbano kati ya viongozi wa shirikisho la soka nchini Sierra Leone dhidi ya waziri wa michezo nchini humo Paul Kamara.

Malumbano kati ya pande hizo mbili yaliibuka kufuatia viongozi wa shirikisho la soka nchini Sierra Leone kumpinga vikali kocha Olof Mattsson anaelipwa mshahara na serikali kufuatia hatua yake ya kukataa kufanya kazi kwa ukaribu na kocha mzawa Christian Cole.

Hata hivyo kumalizika kwa malumbano hayo kumechangiwa na makubaliano yaliyofikiwa na pande hizo mbili ambapo kubwa ni kushirikishwa kwa kocha huyo mzawa katika timu ya taifa na tayari Olof Mattsson ameonyesha kuridhia utaratibu huo.

No comments:

Post a Comment