KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 31, 2011

Paul Scholes ATUNDIKA NJUMU.




Kiungo wa klabu bingwa nchini Uingereza Man Utd Paul Scholes ametangaza kustafu rasmi mchezo wa soka baada ya kupatwa na kigugumiza cha kufanya hivyo kabla ya kumalizika kwa msimu wa mwaka 2010-11.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36, ametangaza kufanya maamuzi hayo huku akiwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Man utd kufanikiwa kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa nchini Uingereza kwa mara ya 19 msimu huu sambamba na kuifikisha klabu hiyo katika hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kabl ya kubanjuliwa na Barcelona mwishoni mwa juma lililopita.

Taarifa iliyothibitisha kuondoka kwa Scholes, imeeleza kwamba hamna budi kufanya hivyo kufuatia muda kufika na lengo lake ni kutaka kuendelea kutunza heshima yake aliyoipata akiwa na klabu hiyo ya Old Trafford, ambayo bado itaendelea kumuhitaji siku hadi siku kutokana na nafasi aliyopewa ya kuwa kocha wa timu ya vijana klabuni hapo.

Taarifa hiyo pia imetoa nafasi za kuwashukuru wale wote waliomuwezesha kiungo huyo kufikia mafanikio aliyoyapata ikiwa sambamba na mashabiki wa soka ulimwenguni kote ambao wamekua wakimfuatilia katika maisha yake ya uwanjani.

Maamuzi ya kustahafu kwa Paul Scholes yamekuja miezi mitatu baada ya aliekua nahodha na beki wa pembeni wa timu ya taifa ya Uingereza pamoja na Man Utd Garry Neville kutangaza kustahafu soka huku akishurutishwa na majeraha yaliyokua yakimkabili mara kwa mara.

Paul Scholes daima atakumbukwa hasa akiwa katika kikosi cha klabu ya Man utd cha vijana toka mwaka 1991-1994 ambapo huko alikuzwa sambamba na wachezaji wengine waliowika na wanaowika kwa sasa na klabu hiyo kama Garry Neville, Ryan Giggs, David Beckham, Nicky Butt pamoja na Phil Neville, kabla ya kupandishwa katika kikosi cha kwanza mwaka 1994.

Akiwa na klabu ya Man utd mpaka hii leo anatangaza kustahafu soka Paul Scholes amefanikiwa kucheza michezo 466 na kupachika mabao 102 huku akitwaa mataji mbali mbali ambapo mataji hayo ni:


Kombe la ligi kuu ya soka nchini Uingereza amechukua mara 10 na hii ni katika msimu wa mwaka 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, pamoja na 2010–11

Kombe la chama cha soka nchini Uingereza FA Cup amechukua mara 3 na ni katika msimu wa mwaka 1995–96, 1998–99 pamoja na 2003–04

Kombe la ligi Curling Cup amechukua mara mbili na hii ni katika msimu wa mwaka 2008–09 na 2009–10

Ngao ya hisani amechukua mara tano na hii ni wa mwaka 1996, 1997, 2003, 2008 na 2010
Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya amechukua mara mbili na hii ni katika msimu wa mwaka: 1998–99 pamoja na 2007–08

Kombe la mabara mara moja na hii ni mwaka: 1999

Kombe la klabu bingwa duniani mara moja na hii ni mwaka: 2008.

No comments:

Post a Comment