KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 24, 2011

PEP GUARDIOLA AWAMWAGIA SIFA MABINGWA WA UINGEREZA.


Wakati hayo yakitokea nchini Uingereza, mabingwa wa soka nchini Hispania Fc Barcelona wameendelea na maandalizi ya mchezo wa hatua ya fainali dhidi ya Man Utd.

Barcelona wameendelea na utaratibu huo huku wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wakijumuika kwa pamoja chini ya meneja wap Josep pep Guardiola Isala.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari meneja huyo wa kimataifa toka nchini Hispania amesema mbali na kufanya mazoezi ya vitendo pia imewachukua siku mbili kutazama picha za televisheni za mchezo wa hatua ya fainali wa msimu wa mwaka 2008-09.

Amesema wamebaini mapungufu yao kupitia mchezo huo uliowakutanisha na Man utd ambao walionekana kuwa bora zaidi ya kikosi chake katika kipindi cha kwanza lakini walifanikiwa kuwashika katika kipindi cha pili.

Hata hivyo Josep Pep Guardiola hakusita kuwamwagia sifa man Utd kwa kusema vbado ni timu bora na yenye uwezo mkubwa wa kutengeneza zaidi ya vikosi vitatu kwa wakati mmoja.

No comments:

Post a Comment