KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 24, 2011

Peter Osaze Odemwingie AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA KLABU.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Nigeria, pamoja na klabu ya West Bromwich Albion ya nchini Uingereza Peter Osaze Odemwingie ameanza mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kusaini mkataba mpya.

Wakala wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amesema uongozi wa klabu ya West Bromwich Albion umefikia hatua ya kufanya mazungumzo na Peter Osaze Odemwingie kufuatia kukunwa na uwezo wake anapokua uwanjani pamoja na na kutaka kumaliza fununu zinazomuhusisha kutaka kuihama klabu hiyo ya The Hawthorns.

David Omigie, wakala wa mshambuliaji huyo amesema mchezaji wake wakati akijiunga na West Bromwich Albion mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2010-11 alisaini mkataba wa miaka miwili ambapo sehemu ya mkataba huo utafikia tamati mwezi August mwaka huu, hivyo inahofiwa huenda akaondoka klabuni hapo akiwa kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu ujao.

Peter Osaze Odemwingie toka alipojiunga na klabu ya West Bromwich Albion akitokea Lokomotiv Moscow ya nchini Urusi, ameshacheza michezo 32 ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza na amefanikiwa kupachika mabao 15 hatua ambayo imemfanya kutangazwa kuwa mfungaji bora wa klabu.

No comments:

Post a Comment