KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 18, 2011

Philippe Mexes - HAKUNA KIFICHO NINAKWENDA AC MILAN.


Beki wa kimataifa toka nchini Ufaransa pamoja na klabu ya AS Roma Philippe Mexes amethibitisha safari yake ya kujiunga na mabingwa wa soka nchini italia AC Milan kuanzia msimu ujao.

Mexes mwenye umri wa miaka 29, ambae amekua na klabu ya AS Roma kwa kipindi cha miaka saba iliyoopita amesema safari yake ya kuelekea mjini Milan ipo kama kawaida na hatua hiyo imekuja kufuatia mkataba wake na klabu ya AS Roma kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Amesema atajiunga rasmi na kikosi cha AC Milan July 12 kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu wa mwaka 2011-12 na imani yake yamtuma kwamba ataendeleza mazuri yaliyopatikana ndani ya klabu hiyo ya mjini Milan hususan kutetea ubingwa uliopatikana msimu huu.

Philippe Mexes pia amesifia maamuzi yake ya kujiunga na AC Milan huku akibainisha wazi kwamba ni klabu kubwa tena yenye historia nzito kama ilivyo kwa klabu za Manchester United, Barcelona pamoja na Real Madrid.

AC Milan kwa kipindi kirefu walihitaji kumsajili beki huyo lakini uongozi wa klabu ya AS Roma uligoma kufanya hivyo hatua ambayo ilimpelekea Philippe Mexes kukataa kusaini mkataba mpya ili aweze kupata nafasi ya kuondoka akiwa kama mchezaji huru.

No comments:

Post a Comment