KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, May 25, 2011

Ryan Giggs AJITOKEZA HADHARANI.


Licha ya kukosekana mazoezini jana, kufuatia sakata la kutembea kimapenzi na mwanadada alieshiriki shindano la Big Brother nchini Uingereza msimu uliopita Imogen Thomas, winga wa kimataifa toka nchini Wales Ryan Giggs alilazimika kucheza mchezo maalum wa kumuaga aliekua beki na nahodha wa klabu ya Man utd Gary Neville uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo.

Ryan Giggs alilazimika kucheza mchezo huo muhimu uliowahusishwa wachezaji wote waliocheza Man utd sambamba na Gary Neville dhidi ya kikosi cha Juventus ya nchini Italia baada ya kujumuishwa kikosini na alikua hana namna ya kukataa utaratibu huo.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 37, ambae pia ni baba wa watoto wawili imebainika alijihusisha na suala la kimapenzi na Imogen Thomas toka mwezi wa tisa mwaka jana, na kwa kutotaka suala hilo lisifahamike, alizimika kwenda mahakamani kwa lengo la kujiwekea kizingiti cha kutokutajwa jina lake katika vyombo vya habari kufuiatia sheria za nchini Uingereza.

kabla ya sakata hilo kufahamika Giggs alikua akitajwa kwa mafumbo na vyombo vya habari nchini humo, hatua ambayo ilimlazimu mmoja wa wabunge wa chama cha Liberal Democrat aitwae John Hemming kutaka sheria hiyo uvunjwe kwa lengo la kutoa haki kwa wanawake kama Imogen Thomas, ambapo pia alilitaja jina mchezaji huyo bungeni.

Katika mchezo huo maalum wa kumuaga Gary Neville, Man utd walikubali kisago cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Juventus ambapo bao la mashetani wekundu lilifungwa na Wayne Rooney huku mabao ya Juve yakifungwa na Simone Pepe pamoja na Manuel Giandonato.

No comments:

Post a Comment